MSAMAHA
Stefano aliwasamehe wauaji wake. Alisema, “Bwana, usiwalaumu kwa sababu ya dhambi hii” (Matendo 7:60). Msamaha ni gharama ya kumfuata Yesu Kristu. Watu hujiandaa kusamehe lakini walio wengi hawajiandai kusamehewa. Je kama unasemehewa unapokea msamaha? Bwana Yesu alipokuwa kufani msalabani alisema maneno saba msalabani: Neno la kwanza ni: “Baba, uwasamehe kwa maana hawajui wanalofanya,” (Luka 23: 34). “Kufanya makosa ni
jambo la kibinadamu, kusamahe ni jambo la kimungu,” Alisema Alexander Pope (1688-1744) mshairi wa Uingereza. Lakini tujue kuwa kuendelea kutenda makosa bila kuacha ni jambo la kishetani. Yesu alivyowasamehe waliomkosea alifanya jambo la kimungu. Hakutaka kutwika uwezo wake wa kukumbuka mzigo mzito wa mambo yaliyopita. Kama yeye alifanya hivyo kwa nini sisi tunabeba mizigo mizito ya mambo mabaya tuliyotendewa.
jambo la kibinadamu, kusamahe ni jambo la kimungu,” Alisema Alexander Pope (1688-1744) mshairi wa Uingereza. Lakini tujue kuwa kuendelea kutenda makosa bila kuacha ni jambo la kishetani. Yesu alivyowasamehe waliomkosea alifanya jambo la kimungu. Hakutaka kutwika uwezo wake wa kukumbuka mzigo mzito wa mambo yaliyopita. Kama yeye alifanya hivyo kwa nini sisi tunabeba mizigo mizito ya mambo mabaya tuliyotendewa.
William Shakespeare aliandika hivi katika kazi yake iitwayo, “The Tempest,” “Prospero, alipopewa nafasi kuwaadhibu wale waliomwondoa katika nafasi yake kama mfalme, alisema, ‘Tusitwishe mzigo mzito kumbukumbu zetu kwa jambo zito ambalo limepita.” Kununa kwetu hakubadili historia. Kukasirika kwetu hakubadili historia. Kulaani hakubadili historia. Kutukana hakubadili historia. Kusamehe kunabadili historia maana hakuongezi idadi ya watu wabaya lakini kulipiza kisasi kunaongeza idadi ya watu wabaya.
Bwana Yesu ni kioo cha jamii na familia katika kutoa msamaha. Aliwatetea waliomfanyia mabaya kuwa hawakujua. Wanafamilia wajifunze toka kwa Yesu kusameheana. Maneno “nisamehe” yawe kama kiitikio katika familia. Familia ni shule ya kwanza ya kujifunza kusamehe na kupokea msamaha. Wazazi ni walimu wa kwanza wa somo la msamaha. Kama pametokea ugomvi, msamaha ufuate kama asubuhi inavyofuata usiku. Ugomvi huanza kwa kutokubali kosa na kuomba msamaha. Mfano, mtu mmoja alimwambia mwenzake, “ulitenda kosa.” Mwenzake alijibu, “sikutenda kosa.” Ugomvi ulianza na marafiki hao wawili walikasirikiana. Mmoja baadaye alisema, “Samahani naomba unisamehe.” “Na mimi naomba nisamehe pia,” alisema mwenzake. Ugomvi ulimalizika, kwa sababu ya maneno machache ya upendo.
Kuomba msamaha na kukubali kupokea msamaha ni tiba. Karl Menninger, daktari bingwa wa magonjwa ya akili kama kichaa alisema kuwa kama angeweza kuwafanya wagonjwa kwenye hospitali ya wagonjwa wa akili kuamini kuwa dhambi zao zimesamehewa, asilimia 75 ya wao wangetoka wamepona siku inayofuata. Mzee Joe alikuwa kufani kwenye kitanda cha mahuti. Kwa muda wa miaka mingi alikuwa hapatani na Bill, ambaye zamani alikuwa mmoja wa marafiki zake. Akitaka kunyosha mambo yake kabla ya kuaga dunia alimtuma Bill waongee na kumaliza mambo. Bill alipofika, Joe alimwambia kuwa anaogopa kwenda mbinguni akiwa na kinyongo naye. Kwa kusita na kwa kujikaza Joe aliomba msamaha kwa mambo aliyoyasema na kuyatenda. Alimwaakikishia Bill kuwa amemsamehe kwa makosa yote aliyomtendea. Mambo yote yalionekana kwenda vizuri mpaka hapo Bill alipojiandaa kuondoka. Alipokuwa anatoka chumbani, Joe alimuita, “Lakini kumbuka, nikipona, haya yote niliyosema hayana maana wala uzito.”
No comments:
Post a Comment