Thursday, 10 March 2016

ASILI YA UPENDO!!!!

UPENDO ASILI YAKE NI MUNGU MWENYEWE!!!!!!!Jamii zetu zimekosa mwelekeo na kuwa na mmomonyoko mkubwa wa maadili kutokana na kukosa upendo. Hii inadhihirishwa na kuongozeka kwa matendo maovu kila leo katika familia zetu, jamii, kanisa na hata nchi kwa ujumla.
Kila moja awe mstari wa mbele kuchukua nafasi yake ili mambo yaweze kusonga mbele.
MWANAUME NI NANI KATIKA JAMII?



o        Mwanaume ni kiongozi wa familia
o        Mwanaume ni mlinzi wa mwanamke pamoja na familia
o        Mwanaume ni mfano wa kuigwa na jamii
o        Mwanaume ni mrithi wa Mungu

MWANAUME MWENYE ASILI YA MUNGU (MWENYE MAADILI MAZURI)

o   Ni mnyenyekevu wakati wote
o   Ni mvumilivu wakati wote
o   Yupo tayari kusuluhisha kesi yake na kuanza upya
o   Ni mwepesi kusamehe na kusahau
o   Ni mtu mwenye utu na anathamini utu wa mtu
o   Anajali watoto na mke wake pia
o   Hatakama atakuwa si muaminifu hujitahidi sana mke wake asijue

MWANAUME MWENYE ASILI YA DUNIA (ASIYE NA MAADILI MAZURI)

o   Ni mkorofi kupindukia
o   Hana utu wala kujali
o   Ni mtu wa lawama wakati wote
o   Hana hofu kwa chochote anachokifanya
o   Huhesabu makosa wakati wote
o   Hana maneno ya faraja kila wakati hulaani tu
o   Hana moyo wa kusamehe, siyo rahisi kesi yake imalizike kwa amani

MWANAMKE NI NANI KATIKA JAMII?
o   Mwanamke ni msaidizi wa mwanaume
o   Mwanamke ni taji ya mwanaume
o   Mwanamke ni mjenzi wa mji wake na nyumba yake
o   Mwanamke ni kipenzi cha watoto na mume
o   Mwanamke ni mwalimu wa familia
o   Mwanamke ni mshawishi wa tabia njema kwa jamii inayomzunguka

MWANAMKE MWENYE ASILI YA MUNGU (MWANAMKE MWENYE MAADILI)

o Hana haraka ya mambo
o Mvumilivu, mnyenyekevu, mtiifu, mkweli, anaheshima, anajituma, ana utu
o Yupo tayari kufanya suluhu na kusahau
o Yupo tayari kujifunza kutokana na makosa
o Ana mapenzi ya dhati naya ukweli
o Anajali watoto na mume wake pia pamoja na jamii yote inayomzunguka
o Hayupo tayari kumsaliti mume wake hata kama sababu zote anazo.

MWANAMKE MWENYE ASILI YA DUNIA (ASIYE NA MAADILI)

o  Ni mkorofi
o  Hasira zake huwa karibu na za wazi wazi sana
o  Kinywa chake hutoa matusi na lawama wakati wote
o  Hukusanya makosa ya mume wake wakati wote
o  Huwa na upendo wa mtego, hana upendo wa dhati
o  Hupenda kupokea zaidi ya kutoa
o  Hulazimisha mambo yafanyike hata kama haiwezekani kwa wakati huo.

MAPENZI NI NINI?
Kutokana na tafsiri mbali mbali na mijadala mbali mbali inaonesha mapenzi ni ‘’ mkusanyiko wa hisia za binadamu zinazopelekea kujenga urafiki wa kudumu kati ya mwanamke na mwanaume au mtu na mtu mwingine.’’mapenzi asili yake ni Mungu 1Yohana 4;7-8 (7Wapenzi na tupendane, kwa kuwa upendo watoka kwa Mungu. Kila apendaye amezaliwa na Mungu naye anamjua Mungu.8 Yeye asiyependa hamjui Mungu, kwa sababu Mungu ni upendo.)

MPENZI NI NANI?
o   Ni binadamu aliyejitoa kwa ajili yako, kusaidiana na wewe katika shida na raha
o   Ni mtu yeyote aliyetayari kuumizwa kwa ajili yako
o   Ni binadamu aliye tayari kushauriana na wewe pale anapoona umekosea
o   Ni binadamu aliyetayari kuona unafanikiwa badala ya kuangauka
o   Ni binadamu aliyetayari kushirikisha hisia zake za kimapenzi na wewe bila kificho

KUFANYA MAPENZI NI NINI?

o   Kuonesha hisia zako za kimapenzi kwa vitendo
o   Kufanya vitendo vya upendo kwa wale wote walio shirikiana na wewe ktika shida au raha
·         Kujitoa kwa jamii nzima zaidi ya kusubiri kupokea Zaidi


KUSUDI LA KUFANYA MAPENZI NI NINI?

o   Kumfurahisha mpenzi wako
o   Kufurahisha mwili wako na nafsi yako
o   Kupata watoto/ kuanzisha familia kwa kupata watoto
o   Kujenga ushirikiano wa kudumu baina yako na mwenzi wako/ jamii inayokuzunguka
o   Kuonesha hisia za mapenzi kwa vitendo na kufanya suluhu ya matatizo yenu.

MAPENZI YANABEBWA NA VITU VIWILI VIKUBWA AMBAVYO NI:
UPENDO NA HISIA ZA MAPENZI.

UPENDO NI NINI?

  Ni tendo la hiari kutoka moyoni mwa mtu analo kusudia kulifanya kupitia vitendo vya ukarimu, upendo siyo kujivuna, siyo kujisikia wewe ni bora kuliko wengine, siyo kulipiza kisasi, siyo kulaani bali kubariki n.k

  Upendo ni kusaidiana katika raha na shida pia kutoa shukurani kwa Mungu na jamii nzima pale unapokuwa umeshirikiana nao katika jambo lako lolote.

  Upendo husaidia kumaliza ugomvi na kufanya jamii nzima iwe na amani

UKWELI KUHUSU HISIA ZA MAPENZI UPOJE?
o   Hisia za mapenzi hujengwa na vitendo vya upendo
·         Hisia za mapenzi huweza kutoweka na kuhamia mahali popote pale penye upenyo ambapo vitendo vya upendo hupatikana kwa urahisi. Ili kudumisha NDOA yenu au mahusiano yenu itakutegemea wewe kama wewe eidha ni mwanamke / mwanaume. Kwa upande wa mwanamke ana paswa kuonesha upendo zaidi kuliko kupokea.

ISHARA ZA KUTAMBUA (UPENDO WA KIMAPENZI) PENZI LA KWELI.
1.     Mtu huyo atakamata umakini wako na atakuvutia (attention).
2.     Atajaa moyoni na mwazoni mwako kuliko kawaida na wengine.
3.     Utatamani sana uwepo wake wakati wote (kuwa naye).
4.     Utapenda kuwasiliana naye mara kwa mara (kama hamko wote).
5.     Utakuwa na moyo wa kumjali, wema, zawadi na kujitoa sana kwa ajili yake.
6.     Utakuwa na heshima ya juu sana, adabu, utii na uaminifu sana kwake.
7.     Utakuwa na maneno mazuri, maneno laini, na maneno ya upendo kwake.
8.     Utakuwa na moyo/uwezo wa kumvumilia au kuchukuliana naye vile alivyo.
9.     Utakuwa na hamu ya kumgusa au kumshika kwa upendo (si tamaa).
10.   Utakuwa na moyo na utayari wa kumlinda na kumhifadhi.
11.   Uhusiano wenu utapendeza mbele za watu wengi (si lazima wote)
12.   Utakuwa na amani na furaha ya ajabu moyoni mwako/mwenu.


Mungu alisema kwa mkono wa Mtume Paulo kuuelezea Upendo kwa namna hii;
1 Cor 13 : 4-8(a)
*         Upendo huvumilia/subira  (Love is patient)
*         Upendo hufadhili/hufanya wema (Love is kind)
*         Upendo hauna husuda (Love doesn’t Envy)
*         Upendo haujivuni (Love is not proud)
*         Upendo haukosi adabu (Love is not rude)
*         Upendo hauna ubinafsi (Love is not selfish)
*         Upendo hauna uchungu (Love is not easily angered)
*         Upendo hauhesabu mabaya (Love doesn’t count wrongs)
*         Upendo haufurahii uovu (Love doesn’t rejoice with evil)
*         Upendo hufurahia ukweli (Love rejoices in truth)
*         Upendo unalinda (love always protects)
*         Upendo huamini yote (Love always trusts)
*         Upendo hutumaini (Love always hopes)
*         Upendo hustahimili (Love always perseveres)
‘’whatever the love you made reflects your internal feeling and ............................“
Hatuishi tu kwa kulima na kufuga bali tunalima na kufuga kwa kufuata kanuni za kilimo bora ili kupata mazao mengi na kufanya kazi zetu kuleta ufanisi mkubwa katika maisha yetu............nakutakia tafakari njema.
Lakini kumbuka mahusiano mazuri yanahitaji kufuata misingi yake kwa mipangilio inayokubalika sio bora mapenzi.
Tofautisha kati ya mapenzi na upendo
Tofutisha kati ya urafiki na mahusiano


By joseph joachim

No comments:

Post a Comment