Thursday, 10 March 2016
ASILI YA UPENDO!!!!
UPENDO ASILI YAKE NI MUNGU MWENYEWE!!!!!!!Jamii zetu zimekosa mwelekeo na kuwa na mmomonyoko mkubwa wa maadili kutokana na kukosa upendo. Hii inadhihirishwa na kuongozeka kwa matendo maovu kila leo katika familia zetu, jamii, kanisa na hata nchi kwa ujumla.
Sunday, 6 March 2016
JE?UNA HURUMA!!!!!
JE HURUMA YAKO NI KAMA HURUMA YA MUNGU?
JUMAPILI YA 4 YA KWARESIMA
1. Yos. 5: 9a, 10 -12
|
2 Kor 5: 17-21
|
Lk 15: 1-3, 11-31
|
Kama kuna nguvu kubwa tuliyo nayo ni nguvu ya kuwa na sura na mfano wa Mwenyezi Mungu. Tuna DNA ya kiroho ya Mungu. Kwa nguvu hiyo tunaweza kuwa na huruma kama Mungu. Mungu haweki kando huruma yake, tusiweke kando huruma yetu. “Wingu jeusi siyo alama kuwa jua limepoteza mwanga wake; na hatia nyeusi sana siyo
Saturday, 5 March 2016
SIKU YA WAPENDANAO ASILI YAKE.......
SAINT VALENTINE

RANGI nyekundu, maua, mishumaa,
alama za moyo, mitoko na mambo mengine ya mapenzi ndio yanayotawala mwezi huu
na hasa leo katika Siku ya Valentine, inayoadhimishwa kuwa ndiyo Siku ya
Wapendanao kwa maana ya mapenzi ya watu wawili; mwanamume na mwanamke.
Hata hivyo, historia ya Siku yenyewe
ya Wapendanao, wala si kwa namna inavyoadhimishwa kuwa siku ya mapenzi hayo ya
wapenzi wawili;
mwanamke na mwanamume. Fadha Frank O’Gara wa Kanisa la
Whitefriars Street la Dublin, Ireland, anaelezea habari ya mtu ambaye ndiye
chimbuko la siku hiyo, Mtakatifu Valentine, ambaye inaelezwa kwamba mabaki ya
mwili wake yamehifadhiwa katika kanisa hilo.
Fadha O’Gara anasema Mtakatifu
Valentine alikuwa Padre wa Kanisa Katoliki, aliyeishi katika karne ya tatu AD,
wakati wa utawala wa Roma wa Claudias. Claudias inaelezwa kwamba alikataza
vijana kufunga ndoa, kwa kuwa aliamini kuwa vijana ambao hawajaoa, ni askari
wazuri na walikuwa wapiganaji wazuri, kuliko vijana ambao wameoa, ambao siku
zote ni waoga katika vita wakihofia familia na wake zao wataishije kama wakifa
vitani.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa jamii
aliyoishi Mtakatifu Valentine, ilikuwa jamii huru katika kujiamulia mambo yao,
ambapo ndoa za wake wengi zilikuwa nyingi kuliko za mke mmoja, ingawa wengi wao
walivutiwa na imani ya Kikristo iliyokuwa ikisisitiza ndoa ya mke mmoja. Pamoja
na kuwepo kwa utamaduni huo, Kanisa Katoliki katika jamii hiyo, lilisisitiza
msimamo wake kuwa ndoa ni jambo takatifu kati ya mwanamume mmoja na mwanamke
mmoja katika maisha yao na hilo lilipaswa kuheshimiwa.
Kwa kufuata msimamo huo wa Kanisa,
Mtakatifu Valentine, akitambua kuwa Claudias amepiga marufuku ndoa kwa vijana,
alianza kushawishi vijana na kuwasaidia kwa siri kufunga ndoa ya mke mmoja kwa
kufuata imani ya Kikristo. Inaelezwa kwamba Mtakatifu Valentine alifungisha
ndoa mpaka za wanajeshi kwa siri, hatua iliyosababisha akamatwe, akawekwa
gerezani na kuteswa kwa kufungisha ndoa kinyume na agizo la Claudius.
*Gerezani
Mtakatifu Valentine alipokuwa
gerezani, simulizi zinaeleza kuwa alionesha baadhi ya miujiza kwa wafungwa
wenzake na viongozi wa magereza. Moja ya miujiza, ulifanyika familia Asterius,
aliyekuwa akisimamia kesi ya kutakiwa kuuawa kwa Mtakatifu Valentine, kutokana
na kosa lake la kufungisha ndoa kwa siri kinyume na agizo la Claudius. Jaji
Asterius alikuwa na mwanawe wa kike aliyekuwa na upofu, lakini kwa maombi ya
Mtakatifu Valentine, mtoto huyo akapona, hatua iliyosababisha Jaji huyo kuwa
Mkristo.
kumuombea Asterius akapona upofu ,
Valentine alihukumiwa huyo kwa kutumia Sheria Roma. Kukatwa kichwa Hukumu dhidi
ya Mtakatifu Valentine, ilitaka achukuliwe hatua tatu za mateso; ya kwanza
apigwe na maaskari, pili apigwe mawe na kisha akatwe shingo kwa sababu ya
msimamo wake katika ndoa za Kikristo.
Inaelezwa kwamba baada ya kupokea
hukumu hiyo, kabla haijatekelezwa Mtakatifu Valentine aliandika ujumbe wa
mapenzi kwenda kwa mtoto wa kike wa Asterius, ambao mwisho ujumbe huo uliishia
na neno; “kutoka kwa Valentine wako.”
Kuna taarifa kwamba Mtakatifu
Valentine alimpenda kimapenzi mtoto huyo wa Jaji aliyemfunga, ndio maana
aliandika ujumbe huo kwake. Fadha O’Gara akielezea mtazamo wake kuhusu
Mtakatifu Valentine alivyokuwa, anasema kuna wakati mtu atalazimika kuonesha
waziwazi anachoamini hata kama yuko karibu na kifo.
*Mabaki ya mwili wake
Mateso dhidi ya Mtakatifu Valentine,
hayakuishia hewani kwani jamii mpaka leo inamkumbuka na Kanisa la Whitefriars
Street Church, ni moja ya makanisa matatu yanayodai kwamba limehifadhi mabaki
ya mwili wa Padre Valentine. Kutokana na madai hayo, leo hii watu wengi
husafiri kwenda kuhiji katika kanisa hilo, kwa heshima ya kumbukumbu ya
Mtakatifu huyo wa Kikristo.
“Sasa Mtakatifu Valentine
anajulikana kama mlezi na Mtakatifu wa wapendanao. Kabla ya kuingia katika ndoa
ya Kikristo, lazima uzingatie maandiko ya Mungu katika maisha yako...unahitaji
uwezo wa Mungu katika maisha yako. “Kama Valentine angekuwepo hapa leo, ambacho
angesema kwa watu walio katika ndoa, kwamba kuna wakati mtakabiliwa na majaribu
na shida mbalimbali katika ndoa, kiasi cha kutishia kutunza kiapo chako cha
ndoa.
“Lakini usishangae mapenzi moto moto
uliyo nayo kwa mume au mkeo, yakabadilika na kupoa na labda kuanza kuingia
katika maisha ya kiutu uzima hivyo ndoa changa, ziwe tayari kukabiliana na
changamoto hizo,” anasema Fadha O’Gara. Anawataka wanandoa, siku ya ndoa yao
kufikiria changamoto hizo,” anasema Fadha O’Gara na kuongeza kuwa; Mapenzi kwa
wanadamu na mvuto wa kimapenzi katika ndoa ni mambo yanayopendeza na
yaliyobarikiwa na Mungu, lakini katikati yake kuna kivuli cha msalaba, na hiyo
ndio maana ya Valentine kwake.
*Sherehe duniani
Siku ya Valentine au Siku ya
Mtakatifu Valentine, imekuwa ikisherehekewa kila Februari 14 ya kila mwaka. Ni
siku ambayo watu huonesha mapenzi yao kwa watu wengine, si lazima wake kwa
waume, bali hata wazazi, watoto na marafiki kwa kuwatumia kadi, maua au
chocolates vikiambatana na ujumbe wa mapenzi.
Kuna baadhi ya jamii, wamejenga
utamaduni wa kila miaka minne, Siku ya Wapendanao wanawake walioolewa hutoa
tamko la kudumisha ndoa na mumewe. Pia kuna taarifa kwamba Siku ya Wapendanao,
ni utamaduni wa Waroma uliokuwepo kabla ya Mtakatifu Valentine mwenyewe, ambapo
kulikuwa kukifanyika sherehe.
Inaelezwa kwamba Waroma walikuwa na
sherehe iliyoitwa Lupercalia iliyokuwa ikifanyika katikati ya kila Februari,
wakati wa kuanza kwa majira ya joto. Katika sherehe hizo, wavulana walikuwa
wakiletewa vikasha vyenye majina ya wasichana na kutakiwa kuokota karatasi na
kutaja jina la msichana katika karatasi husika. Baada ya kutaja jina hilo,
mvulana huyo alipaswa kuwa rafiki na msichana husika na wakati mwingine
ukubwani, wako walioendeleza urafiki wao mpaka katika ndoa.
Inaelezwa kuwa baadaye, Kanisa
lilidhamiria kubadilisha sherehe hizo kuwa za Kikristo na kuamua kuzitumia
kumkumbuka Mtakatifu Valentine. Baadaye, jina la Mtakatifu Valentine, likaanza
kutumiwa na jamii katika kuelezea hisia zao kwa watu wanaowapenda.
Kwa sasa siku hiyo ya Mtakatifu
Valentine, imekuwa ikisherehekewa kila february 14 karibu dunia nzima, ingawa
katika nchi na mataifa mengi ikiwemo Tanzania, inasherehekewa lakini si siku ya
mapumziko, ingawa mwaka huu imeangukia siku ya mapumziko. Imetafsiriwa kutoka
vyombo mbalimbali vya habari.
By joseph Joachim
josejoachim01@gmail.com
http://thejoses01.blogspot.com/2016/03/siku-ya-wapendanao-asili-yake.htmlFriday, 4 March 2016
GHARAMA YA KUMFUATA KRISTU
MSAMAHA
Stefano aliwasamehe wauaji wake. Alisema, “Bwana, usiwalaumu kwa sababu ya dhambi hii” (Matendo 7:60). Msamaha ni gharama ya kumfuata Yesu Kristu. Watu hujiandaa kusamehe lakini walio wengi hawajiandai kusamehewa. Je kama unasemehewa unapokea msamaha? Bwana Yesu alipokuwa kufani msalabani alisema maneno saba msalabani: Neno la kwanza ni: “Baba, uwasamehe kwa maana hawajui wanalofanya,” (Luka 23: 34). “Kufanya makosa ni
Subscribe to:
Posts (Atom)