JIFUNZE
KUBADILIKA, JIFUNZE KUFIKIRI, JIFUNZE KUTENDA, JITIE ROHO YA MUNGU, AMINI
KUPATA NA KUKOSA.
SOMA
KUSOMEKA!!!!!!!!
ALEX ni kijana mwenye umri wa miaka 30.Ana shahada ya uzamili (Masters) ktk
masuala ya Usimamizi wa biashara, na kwa sasa anafanya kazi kama Mkurugenzi wa fedha kwenye shirika moja lakimataifa hapa nchini.Hajaoa bado, lakini ana
nyumba mbili nzuri za kuishi hapa jijini. Moja MbeziALEX ni kijana mwenye umri wa miaka 30.Ana shahada ya uzamili (Masters) ktk
masuala ya Usimamizi wa biashara, na kwa sasa anafanya kazi kama Mkurugenzi wa fedha kwenye shirika moja lakimataifa hapa nchini.Hajaoa bado, lakini ana
Beach na nyingine Kimara.. Ana gari 2 za kutembelea na 3 za biashara.. Anamiliki duka moja la nguo Kariakoo na jingine la simu Mlimani city. Ni mcha Mungu, mpole na mtanashati.. Ni miongoni mwa vijana waliofanikiwa kimaisha.ALEX ana rafiki yake aitwae MUGGY..Huyu ni Afisa Mtendaji mkuu (CEO) wa Shirika moja la ndege hapa nchini. ALEX na MUGGY wamekua marafiki kwa muda mrefu.. tangu utotoni..Wamekua pamoja, wamesoma pamoja tangu chekechea hadi chuo kikuu. Hata masomo yao ya juu (masters) walisoma pamoja Marekani licha ya MUGGY kupata ufadhili Australia, lakini alikataa kwenda ili tu akasome na ALEX Marekani. Walipendana kama mapacha licha ya kuwa hawakuwa ndugu wa damu. Ukimkosea ALEX umemkosea MUGGY and its vice versa.!Waliitwa mapacha walipokua shuleni kwa namna walivyopendana. Kila mmoja alimheshimu mwenzie na kila mmoja
alijitahidi asimkwaze mwenzie..Kila mmoja amefanikiwa kutokana na
juhudi za mwenzie.. upendo wao ulikua wa kweli kutoka kwenye vilindi vya mioyo yao.. Walimpenda Mungu na wote walikua viongozi wa jumuiya za vijana makanisani mwao.Baada ya kuona wamefanikiwa kimaisha
ALEX akashauri watafute wenzi wa maisha...that means waoe.. MUGGY
akasema anahofia kuoa kwa haraka kwani anaweza kupata mke atakayeharibu
urafiki wao.. Mke asiyejua walikotoka nahivyo kuleta mfarakano baina yao...
Akamshauri ALEX wasubiri kwanza hadi WAKATI WA BWANA ULIOKUBALIKA..
ALEX hakumuelewa MUGGY kbs, na akadai tayari ana mchumba na
anampenda sana.. MUGGY akamuuliza kwa muda gani wamekuwa pamoja, ALEX akajibu miezi 6.MUGGY akasema Miezi 6 haitoshi kumchunguza mwenzi wa maisha lakini ALEX akasisitiza anampenda...Mipango ya harusi ikafanyika na MUGGY akachagua kuwa mwenyekiti wa kamati ya harusi ya ALEX.. Lengo lake likiwa kusimamia harusi ya rafiki yake na
kuhakikisha inafanikiwa. ALEX akamshauri MUGGY "tafadhali nawe tafuta mwenzi uoe ili usiwe mpweke. Nidhahiri sasa nitakua karibu zaidi na mke
wangu kuliko wewe. Majukumu ya kifamilia nayo yatanibana, hivyo tafuta
mwenzi ili upunguze upweke..."MUGGY akajibu "Nimemuomba Mungu
anipe mke atakayenifaa.. Bado nasubiri jibu lake. Siwezi kuoa ili tu niepuke
upweke,.maana ndoa ni zaidi ya kuondoa upweke.. Nahitaji mwenzi wa maisha,sihitaji mtu wa kuniondolea upweke.."Siku moja ALEX akiwa katoka MUGGY akampigia simu kuwa yupo nyumbani kwake. ALEX akamuomba amsubiri maana yuko mbali kidogo ila atarudi. Mke mtarajiwa wa ALEX nae alikua nyumbani kwake, hivyo ALEX akamshauri MUGGY apige story na shemeji yake hadi atakaporudi. Lakini ALEX aliporudi nyumbani hakumkuta MUGGY, akamkuta mchumba wake analia.. alipomuuliza kulikoni
akasema MUGGY alijaribu kumbaka...ALEX akawaka kwa hasira... kwa kuwa
alimpenda sana mchumba wake na kwa kuwa hakumkuta MUGGY nyumbani
akaamini maneno ya mchumba wake. Akiwa amechanganyikiwa akaendesha gari kwa kasi kwenda kwa MUGGY. Ile kufika
akamkuta MUGGY kajilaza kwenye sofa. Lakini kabla hajamuuliza chochote,
akampiga kichwani na chupa ya mvinyo aliyokua ameshika mkononi... MUGGY
akaanguka na kuzirai..Akakimbizwa hospitalini ambako ilionekana amepata athari kubwa ndani ya kichwa hivyo alihitaji upasuaji..ALEX akiwa amefura kwa hasira akarudi nyumbani kwa mguu na kuiacha ile gari kwa MUGGY, maana alipewa zawadi na MUGGY siku ya birthday yake.. hivyo akamrudishia zawadi yake maana aliona mtu aliyejaribu kumbaka mchumba wake
hawezi kumpa zawadi. Kwa kuwa hakuwa na gari aliweza kuingia
hadi ndani bila mchumba wake kumsikia wala kumuona... Alipofika akamkuta
anaongea na simu "yes Jenny nimemkomesha.. atajuta kukukataa...Nim
emwambia ALEX kuwa alitaka kunibaka, ALEX akawaka hasira na kwenda
kumfuata... najua huko ni kivumbi na jasho na urafiki wao utaisha leo shosti..."
Alipomaliza kuongea na simu na kugeuka akamuona ALEX.. Akapanick maana
hakutegemea...ALEX akamwambia usiseme lolote maana
nimesikia yote. Kumbe Jenny alikua rafiki yake mchumba
wa ALEX.. Na alipenda kuolewa na MUGGY lakini MUGGY alimkataa ili
kulinda urafiki wake na ALEX.. sasa ile hasira ya kukataliwa ndo wakapanga
kuwafarakanisha..ALEX alipojua ukweli akajilaumu sana kwa
maamuzi ya haraka aliyochukua.. akiwa mnyonge,.na majuto moyoni akakimbia hospitalini ili akamuombe MUGGY
msamaha. Alipofika akakutana na nesi akamzuia..ALEX akapaza sauti huku akibubujikwa na machozi "tafadhali naomba niruhusiwe nikamuombe MUGGY msamaha.. Najua amepoteza fahamu na hawezi kunisikia. Lakini naamini nafsi yake itanisikia na kunisamehe kwa ukatili niliomtendea..Ooh MUGGY my friend urafiki wetu wote nimeshia kukupeleka ICU..Nisamehe sikujua[C1] ..."akalia kwa uchungu ALEX. Mara daktari akatokea. ALEX kwa shauku akamuuliza "dokta MUGGY anaendeleaje??"Daktari akamuangalia ALEX kwa huruma kisha akasema, "Nasikitika kukujulisha kuwa MUGGY amefariki dakika chache
zilizopita baada ya damu nyingi kuvujia kwenye ubongo.."Kisha akaongeza "tumejitahdi kwa kadri ya uwezo wetu kuokoa maisha yake lakini imeshindikana.."ALEX akakamatwa na kutupwa gerezani anakotumikia kifungo cha maisha..MORAL OF THE STORY..!Kuwa makini unapotafuta mwenzi wako
wa maisha. Wengi huharibu mahusiano yao na rafiki zao, ndugu zao au wazazi
wao kisa wameoa/kuolewa.Usiruhusu mke/mume awe chanzo cha
uadui kati yako na ndugu zako, wazazi au rafiki zako. Ukiona mke/mume ni chanzo cha uadui na ndugu zako ujue huyo mke/mume ana roho ya mfarakano (spirit of confusion). Pili, unapopata tatizo kwenye mahusiano kuwa na subira.. Usiharakie kufanya maamuzi. Mara zote maamuzi ya haraka humgharimu mtu baadae. Ona ALEX ktk umri mdogo wa miaka 30, anaenda kumalizia gerezani maisha yake yote yaliyobaki hapa duniani. Mali zake, elimu yake, cheo chake,
heshima yake na vyote alivyovijenga maishani ni kazi bure, just for a single
mistake. Bila shaka huko gerezani alipo anatamani siku zirudi nyuma ili afanye
maamuzi mbadala lakini haiwezekani tena... It’S over and out..!!Mungu akubariki unayesoma ujumbe huu. Kama umeoa/kuolewa amuondolee
mwenzi wako Spirit of Confusion, na kama hujaoa upate mke/mume asiye na spirit of confusion. Upate mtu atakayewapenda rafiki zako, ndugu zako na wazazi wako na kuwathamini..Kumbuka "asiyewapenda wa kwao ni mbaya kuliko asiyeamini.."Hivyo tumuombe Mungu umpate atakayewapenda wa kwenu. Stay blessed.!!
Jua kilichowatokea mke wake Alex na Jenny……………………………………………………………………………… INAENDELEA
COMING SOON!!!!!!!!
By Joseph Joachim
|
0762
969 463 josejoachim01@gmail.com
Usikubali watu wajifunze kupitia mapumgufu yako ruhusu mijadala kupitia mafanikio yako nawe uwe hodari wa kutafuta na kumtegemea MUNGU kwa kila unachokifanya ili kuleta ufanisi wa mambo yako!!!!!!!!!!!
ReplyDelete